Sunday, November 6, 2011

Haijapata kutokea---- Thomas Nyimbo avunja ngome ya CCM Njombe Aweka Rekodi!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgORk-dmfO6NnGdrt6dcJbHBl7ZVFVXkvoYosTQnhBJf70GgRsN40yb-NV8AoNFX6lDi-Eyw6tvn-VFBI9XrnpC9UMEtlQ54EJw0b1BVQHMbb-eaG7zVWLpp-kKBXKDdBxmXKeLaFMdg-Y1/s1600/NYIMBO.JPG
PICT0406.JPG‎Picha ya ofisi mpya ya CHADEMA jimbo la Njombe Magharibi
Wote tunajua mambo ya ajabu yaliyofanywa na CCM wakati wa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010 katika Jimbo la Njombe Magharibi. Baada ya kufanyiwa hujuma ndani ya CCM na baadae akigombea kwa Chadema Thomas Nyimbo aliamua kutokwenda mahakamani na badala yake aliamua kukata rufaa kwa wananchi.
Kwa ufupi CCM Njombe Magharibi iko taabani na ushahidi ni ofisi hii ambayo Mh.Nyimbo nbaada ya kufanikiwa kupata wanachama katika Wilaya nzima ya Njombe (Wanging'ombe) sasa amejenga ofisi hii ambayo sijapata kuiona katika Mikoa mingi iliyopiga hatua kimageuzi. Hii ni ofis ya Wilaya mpya ya Wanging'ombe .
Baadhi ya Majibu ya Wadau haya hapa
Yeye alisema yupo tayari kuwa Mlezi wa Chama wa Mkoa mpya wa Njombe so na hataki mkuwa kwenye ngazi yoyote ya maamuzi ila kushikiri kujenga Chama. Mpaka sasa amenunua pikpiki 8 kwa ajili ya uenezi katika Wilaya mpya ya Wanging'ombe na ameshagharimia safari za waenezi walioenda hadi Ludewa na Makete. Huyu Mzee ni mfano wa kuigwa sana

Kwa kweli huyu mzee ni mfano wa kuigwa maana anakijenga chama na hapo hapo analeta maendeleo kwa wananchi tena akiwa nje ya bunge sipati picha kama angekuwa mbunge wananchi wa jimbo hilo wangepata maendeleo makubwa! Miaka 4 siyo mingi kama Mungu akimpa uhai na nguvu.

Nilipita huko Njombe september Mzee Nyimbo amekuwa akifungua matawi kijiji kwa kijiji na kuvunjavunja ngome ya CCM mpaka sasa bendera za CHADEMA zinapepea kila kijiji na ndani ya vitongoji, kikubwa ni wadau kumpa support katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili tusimike wenyeviti wa vitongoji na vijiji wa kutosha ili kusafisha njia ya 2015. Lengo ni kusajili T2015CDM.

No comments:

Post a Comment